-->

Baraka The Prince Amsajili Lord Eyes

Msanii Baraka The Prince ametangaza rasmi kuanzisha label yake na kutaja wasanii wakubwa wawili ambao wapo chini ya label yake hiyo.

Baraka The Prince (Kushoto) akiwa na Lord Eyez

Akiongea katika kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio Baraka The Prince amesema kuwa rasmi rapa Lord Eyes amesaini chini ya label yake inayofahamika kama ‘BANA’  na kusema ameamua kumchukua Lord Eyes kutokana na uwezo wake.

“Saizi tayari chini ya Label yangu nina wasanii watatu, yupo Lord Eyes, Naji pamoja na msanii mwingine wote hawa wameshafanya kazi zao na zipo tayari tunasubiri tu mwaka ugeuke ili tuanze kuachia kazi. Niliamua kumchukua Lord Eyes kwa sababu kwanza ni rapa mzuri ana uwezo mkubwa na anabadilika sana, lakini pia nimefanya naye kazi katika show mbalimbali ana mashabiki wengi sana”. Alisema Baraka The Prince

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364