Baraka The Prince Asita Kuingia Kwenye Filamu
Msanii Baraka The Prince anayetamba na wimbo wake wa ‘Niache Niende’ amesema wakati wake ukifika naye atajiingiza katika mambo ya filamu nchini kama alivyokuwa Hemed PHD.
Msanii huyo ameelezea hisia zake kwa kile anachokiamini kwa kusema yupo katika harakati za kujenga ‘brandy’ yake ya muziki ili itambulike vizuri katika soko huku akidai alishawahi kufuatwa na director mkongwe katika tasnia ya filamu maarufu kwa jina la Mtitu.
“Nilishafuatwa kabisa na yule ‘director’ Mtitu aliyemtoa Kanumba alikuwa anataka tufanye ‘series’ mimi niwe ‘starling’ na Irene Uwoya lakini kwa kipindi kile sikuwa ‘ready’ kuingia kwenye mambo ya ‘movie’ lakini bado sijawa ready kwasasa hivi kwasababu bado najenga Brandy yangu”. Alisema Baraka
Aidha Baraka amesema endapo siku watanzania watasikia msanii huyo ameingia rasmi huko basi wajue itakuwa moto wa kuotea mbali kwa kuwa hata video zake za muziki anazozitengeneza huwa anaigiza sana.
Kwa upande mwingine ‘hitmaker’ huyo amesema hakuna ukweli wowote unaohusiana baina ya maisha yake na mashairi anayoyatumia katika wimbo zake huku akisisitiza kuwa anaimba kutokana na vitu vinavyotokea kwenye jamii inayomzunguka.