Uzazi Unampenda Monalisa
KATI ya wasanii ambao kila ukutanapo uvutia kwa muonekano wake si mwingine bali ni mwigizaji nyota isiyochuja miaka na miaka Monalisa ni msanii ambaye amekuwepo katika tasnia kwa miaka mingi lakini bado yupo katika muonekano huku mabinti wakija na kuchuja kimuonekano na sanaa yenyewe pia.
Nendeni Duniani mkajaze Ulimwengu ni maneno yaliypo katika maandiko matakatifu yanaendana na wale wanaotii mwigizaji wa filamu Bongo Yvonne Cherryl ‘Monalisa’ anasema kuwa siri kubwa ya kuwa mrembo ni uzazi kila anapotoka kwenye uzazi ndio anazidi kupendeza kwani uzazi unampenda.
“Nashukru Mungu nimekuwa nikizidi kupendeza kila uchwao hasa nikitoka katika uzazi kama unavyoniona nipo mrembo ni jinsi ya kujitunza kama mzazi huwezi kuzeeka kisa uzazi,”alisema Monalisa.
Monalisa ni mmoja kati ya wasanii wakongwe wasiochuja kuanzia uigizaji hadi muonekano kwani siku zote amekuwa aking’ara kwenye filamu huku akiwa bado akionekana ni binti msanii huyo mtoto wake wa kwanza alizaa na mtayarishaji wa filamu marehemu George Tyson.
Filamu Central