-->

Baraka The Prince Hakuniangusha – Alikiba

Msanii Alikiba amefunguka na kusema kuwa msanii Baraka The Prince hakumuangusha kabisa kwenye wimbo wao wa pamoja ‘Nisamehe’

baraka89

Alikiba amesema kuwa kwake yeye ilikuwa rahisi sana kukubaliana na wazo la Baraka kwa kuwa msanii huyo kwanza anakipaji kikubwa lakini pia ni watu ambao wanaendana katika kazi.

Alikiba alisema haya kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kudai Baraka The Prince anapita sehemu alizokanyanga yeye ndiyo maana imekuwa rahisi wao kufanya kazi ya pamoja ambayo mwisho wa siku imeweza kuwa nzuri na kila mmoja amepita vizuri.

“Nisamehe ni collabaration ya kwanza kwangu kwa mwaka huu, wimbo una hisia sana. Mimi nilifurahi sana Baraka aliponipa ‘Idea’ akaniambia ‘Brother’ kuna wimbo nataka tufanye nikausikiliza, yaani hakuniangusha kabisaa jinsi yeye mwenyewe alivyoimba vizuri ilinifurahisha sana na ikawa rahisi kwangu kuingia kwa sababu siku zote Baraka huwa anapita nilipokanyaga na ana ‘talent’ sana kwa hivyo ilikuwa rahisi kufanya kama ambavyo unaweza kuona kazi imetoka ipo vizuri na ‘Chemistry’ ipo vizuri yani mtu hawezi kuwa na mashaka hapo ni lazima ‘featuring’ ingefanyika tu maana siku zote kuna vipaji ambayo vinaendana, huwezi kutoka na kwenda kufanya kazi na mtu mwingine harafu ikaonekana umemfunika au vipi lakini Baraka amefanya vizuri” alisema Alikiba

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364