-->

Wema Awavaa Wanaomsema Vibaya Aunt Ezekiel

SUPA-STAA Wema Isaac Sepetu ‘Madam’, amefunguka kuwa anachukizwa na watu wanaomtolea matusi muigizaji mwenzake, Aunt Ezekiel, baada ya kuhudhuria sherehe ya kuzaliwa ya mzazi mwenza wa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.

wema45

Akizungumza na Za Motomoto News, Wema alisema unatakiwa ufike wakati watu waelewe na waongozwe kwa akili zao za kuzaliwa kwa sababu hakuna kitu kibaya ambacho amekifanya Aunt, kwa kuwa staa mwenzake huyo kwa sasa ni mmoja wa familia hiyo.

“Jamani hebu naomba kwanza wamuache Aunt, hana kosa lolote, hata kama ningekuwa mimi hapa nisingeweza kuacha kwenda kwa sababu tayari ni familia na hawezi kumuacha mumewe aende peke yake maana vitu vingine ni vya kujiongeza tu, nachukizwa sana na jinsi wanavyomrushia maneno ya kashfa,” alisema Wema.

zari022

Aunt Ezekiel akiwa na Zari

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364