Barnaba: Sina Mpango na Kolabo ya Nje
MSANII wa Bongo Fleva, Elias Barnaba, amesema hana mpango wa kufanya kolabo na msanii wa nje kwa sasa kwa kuwa bado anajipanga vizuri kisanaa.
Alisema si kwamba anaogopa ila kwa upande wake anaona bado anahitaji kujipanga zaidi ili atakapoamua kufanya kolabo yoyote iwe kubwa kama alivyorekodi na msanii wa Uganda, Jose Chameleone.
“Muziki hautaki kubahatisha, mimi ni mwanamuziki ninayeongoza kwa kufanya shoo nyingi nje ya nchi, lakini sijataka kumshirikisha msanii yeyote wa nje kwa kuwa muziki wangu bado nauandaa, unaenda kidogo kidogo na nikiona umefika ninakotaka nitafanya hivyo,” alisema Barnaba.
Alisema kufanya hivyo hakumaanishi yeye ni msanii mdogo, ila katika maisha kila kitu lazima ufanye kwa malengo na baada ya wimbo wa ‘Love boy’ anatarajia kuachia wimbo wake mpya wa ‘Alone’.
Mtanzania