Vanessa Mdee Aendelea Kushikiliwa Central
Dar es Salaam. Kamishna wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Siro amesema jeshi hilo bado linamshikilia Msanii maarufu wa mziki wa kizazi kipya, Vanessa Mdee ambaye alikamatwa juzi (Jumatano) kwa tuhuma za matumizi za dawa za kulevya.
Vanessa alikuwa miongoni mwa watuhumiwa wa matumizi ya dawa za kulevya waliotajwa na Mkuu mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika orodha yake ya pili na kuwataka kuripoti katika kituo cha kituo kikuu cha polisi.
Hata hivyo Vanessa hawakuweza kufika kituoni hapo kwa wakati kwa sababu wakati agizo hilo likitolewa alikuwa nje ya nchi na kumtuma mwanasheria wake kumwakilisha.
“Juzi tulimkamata Vanesa Mdee na taarifa zinaonyesha ni mtumiaji na msambazaji lakini upelelezi unaendelea na ukikamiliki tutamfikisha mahakamani au tutamuachia. Na sio hao tu wapo wengine ambao tuna majina baadhi tumewakamata inasemekana huwa wanasafirisha dawa hizo kwenda Afrika Kusini,”amesema Siro.
By Ephrahim Bahemu, Mwananchi ebahemu@mwananchi.co.tz