-->

Batuli:Wasanii Wengi Wanaishi Maisha ya Kuigiza

MKALI wa filamu nchini, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’, amesema hataki watoto wake wawe waigizaji kwa kuwa kuna mambo mengi anayokutana nayo na hataki wakutane nayo.

batuli356

Yobnesh Yusuph ‘Batuli’

Akizungumza na MTANZANIA, Batuli alisema hataki watoto wake, Samir na Malima, wawe waigizaji kwa kuwa amekutana na mambo mengi mabaya yakiwemo kutukanwa mitandaoni, kupandishiwa bei za vitu kiasi kwamba vinasababisha wakati mwingine aishi maisha ya kuigiza.

“Wasanii wengi Tanzania wanaishi maisha ya kuigiza hivyo sitaki watoto wangu waishi katika sanaa kwa sababu wanaweza kuishi kwa kuigiza, nataka wafanye shughuli nyingine nitawasaidia wafikie malengo yao kupitia elimu,” alisema Batuli.

Batuli aliongeza kwamba urithi pekee anaotaka kuwaachia watoto wake ni mali na elimu huku akiwahasa watoto nchini wasome kwa bidii kwa kuwa elimu ndiyo kila kitu katika maisha.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364