-->

Ben Pol Afungukia Ishu ya Ebitoke

Msanii Ben Pol ambaye inasemekana alikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na mchekeshaji Ebitoke, sasa hivi anaonekana kumuepuka msanii huyo kwa sababu ambazo hazijajulikana kwa haraka, kitendo kinachoonesha kumuumiza kihisia Ebitoke.

Ben Pol ambaye alitafutwa kwa kipindi kirefu na mwandishi wetu na kufanikiwa kumpata kwa shida kutokana na ubize aliosema  anao kwa kipindi hiki, alipomueleza kwamba anataka kuzungumzia kuhusu Ebitoke na kwa nini hapokei simu za mchekechaji huyo, Ben Pol alijibu kwa mkato huku akisema kwamba ‘issue’ za Ebitoke zinamkata ‘stimu’.

“Sasa hivi nipo ‘busy’ sana kwa sababu nafanya mazoezi ya ‘show’, lakini kiukweli habari za Ebitoke zinanikata ‘stimu’ kabisa, ‘so’ nikitulia naweza nikakucheki”, alisikika Ben Pol akimjibu mwandishi wetu.

Wiki iliyopita Ebitoke alikuwa kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, na kulalamika kuwa msanii huyo ambaye alikiri kuwa na hisia naye za kimapenzi sasa hivi hapokei simu zake, na wala hajibu ujumbe mfupi anaomtumia katika simu yake, hivyo akaomba watu wamsaidie kumuuliza Ben Pol, kwa nini amefikia uamuzi huo.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364