Lulu Diva Amkataa Nay wa Mitego Hadharani
WAKATI mtaani kukiwa na hapa na pale kuhusu uwepo wa uhusiano Nay Wa Mitego na Lulu Diva, katika moja ya mahojiano na kituo cha habari, Lulu ametoa povu zito kwenda kwa Nay.
“Nay hawezi kuwa type yangu hata siku moja na haijawahi na hawezi kuja kuwahi hata siku moja eti niwe na Nay,”
“Kwanza hajawahi nivutia na kamwe hawezi kunivutia, hivi mimi kweli niwe na Nay haiwezekani kabisa kwa mwanaume kama Yule,” aliongeza.
Pia Lulu alifunguka juu ya mapenzi yake na Wizkid walivyopotezeana huku akisema hakuna kitu anachokikumbuka kutoka kwa staa huyo wa Nigeria.
Mwanaspoti