Ben Pol Akanusha Kutoka na Ebitoke
MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Benard Paul maarufu Ben Pol, amefunguka na kusema hana uhusiano wowote na msanii mwenzake Ebitoke, ila watu wameamua kujipa majibu wenyewe.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Ben Pol alisema watu wameamua kuongea maneno wanayoona yanaweza kuwapa majibu sahihi lakini yeye ameamua kukaa kimya na muda ukifika ataweka wazi kila kitu kama ni kiki au la.
“Mashabiki zangu watulie tu majibu sahihi nitawapa muda ukifika, nafahamu watu wengi wanaongea wanavyoona wao, lakini mimi na Ebitoke hakuna chochote,” alisema Ben Pol.
Aliongeza kuwa hata familia yake haijamshauri chochote wala kumuuliza kuhusu swala hilo ila na wao wanasikia na kuona kwenye mitandao ya kijamii.
Mtanzania