-->

Wema Sepetu Awa Mbogo kwa Polisi

Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu ametoa yake ya moyoni na kutoa tuhuma kwa jeshi la polisi nchini kufuatia baadhi ya polisi kumpiga ndugu yake ambaye jana alikwenda naye mahakamani kusubiri kesi ya Tundu Lissu.

Wema Sepetu anasema kuwa ndugu yake huyo kwa sasa anapatiwa matibabu hospitalini kufuatia kipigo alichopata kutoka kwa polisi hao kwa kile anachosema kuwa kijana huyo alipigwa kufuatia kupita katika mlango wa mahakama.

“Ninachojua mimi ni kwamba binadamu ana haki ya kwenda mahakamani kusikiliza kesi ya ndugu yake… Imeniuma sana kilichomtokea kaka yangu jana, Only now nakuja kujua kwamba alichukuliwa na polisi wakaenda kumpiga mpaka sasa yupo hospitali amelazwa. Kosa lake ni kupita pale mlango wa mahakamani na akasema kabisa yupo pamoja na mimi na mama yangu” alisema Wema Sepetu

Hata hivyo Wema Sepetu anasema wakati anasubiri kesi ya Tundu Lissu jana mahakamani alikuja kuitwa na polisi na kuambiwa kuwa aondoke eneo hilo na arudi nyumbani kwake

“Maana jana tulivyokuwa tumekaa tunasubiri kesi ya Mh. Tundu Lissu itajwe, Nilikuja kuitwa walitaka niondoke eneo hilo na nirudi nyumbani… Nilikuwa mkali kidogo, wakanijia na huyo kaka yangu ambaye alisema kuwa yupo pamoja na mimi” alisema Wema Sepetu

Mbali na hilo Wema Sepetu alisema kuwa namna ambavyo jeshi la polisi linafanya si jambo zuri na kusema matendo ya namna hii yanaweza kuleta shida au matatizo siku za usoni

Mwishoni mwa mwezi wa pili mwaka huu msanii Wema Sepetu alifanya maamuzi magumu na kuamua kuhama chama kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuhamia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) baada ya msanii huyo kutuhumiwa na serikali kuwa anajihusisha na Uuzaji na matumizi ya madawa ya kulevya. Ambapo mpaka sasa bado kesi yake inaendelea katika Mahakama Kuu Tanzania (KISUTU)

EATV.TV

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364