Bodi ya Filamu:Hakuna Wezi wa Kazi za Sanaa
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi. Joyce Fisso amesema hana taarifa na wizi wa kazi za wasanii na kuwasihi wasanii kufikisha malalamiko yao ofisini kwake ili yaweze kufanyiwa kazi kwa wakati.
Akiongea ndani ya eNewz Bi.Fisso amesema kama kuna wasambazaji wanaohusika na wizi wa kazi za wasani au mtu yeyote ni bora kuacha mara moja kufanya kazi hiyo kabla mkono wa sheria kumfikia na kuchukua hatua dhidi yake.
Pia Bi. Fisso alitoa pongezi nyingi kwa kampuni ya EAST AFRICA TELEVISION LIMITED kwa kuanzisha tuzo ambazo zina vipengele vya muingizaji bora wa kike, wa kiume na movie bora ya mwaka na kusema tuzo hizo zitaongeza hadhi kwa wasanii watakaoshinda na kuongeza chachu kwa wasanii wengine kufanya kazi zenye ubora zaidi.
eatv.tv