-->

Bongo fleva Haitapoteza Muziki wa Dansi – Nyoshi

Msanii wa dansi nchini Tanzania Nyoshi amesema muziki wa bongo fleva haujaua soko la muziki wa dance nchini ila kwa sasa kuna baadhi ya wadau wa radio na televisheni wameamua kusapoti muziki wa bongo fleva zaidi.

nyoshi

Akiongea ndani ya eNewz Nyoshi amesema bendi nyingi zinatoa nyimbo kwa wakati lakini ukipeleka nyimbo kwenye televisheni na radio hazipigwi kwa kuwa tayari baadhi ya wadau kwenye vyombo vya habari wanasapoti aina fulani ya muziki hivyo wanatumia muda mwingi kufikiria kwa sasa wafanye nini ili kuinua muziki wa dansi.

Nyoshi amesema hata kama ukifanya video nje ya nchi haiwezi kupigwa kwa kuwa baadhi ya vyombo vya habari kwa sasa vina wasanii ambao wanawabeba wakidhani kwamba ndiyo watakao waingizia hela hivyo bado sapoti wanayoipata  ni ndogo na  kuwasihi mashabiki zake kuomba nyimbo zao kwa wingi kwenye radio na TV.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364