-->

Bongo Movie Full Kutishana Tico Atumiwa Sms za Mikwara

KUFUATIA kuyumba kwa soko la filamu na kufanyika kwa mikakati mbalimbali ya kutafuta suruhu la kuokoa soko hilo lilopotezwa na filamu za nje, sasa wasanii na watayarishaji wameanza kutishana wao kwa wao ikiwa kuambiana watafapotezana katika tasnia ya filamu.

Mmoja kati ya watayarishaji wa filamu Bongo Timoth Conrad ‘Tico’ aliposti katika ukurasa wake andiko na kurekodi video na kuirusha youtube akitoa taadhari kuwa kutoa filamu kutoka nje si suruhu ya kujenga filamu za ndani, alijikuta akipingwa na watayashaji wenzake wengi wakidai anapotosha.

“Filamu zetu zina matatizo mengi hivyo tunatakiwa kujitathimini wenyewe sasa wanaonifuata inbox facebook kunitishia msiendelee hainifanyi kuacha coz naitakia mema tasnia ya filamu,” alisema Tico.

Awali alikuwa Tico pekee akijaribu kuongelea suala la ubora wa filamu zetu na si kwa sababu ya sinema kutoka nje hivi karibuni wasanii walifanya maandamano na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali na kuzua mjadala baada ya Rais wa Taff Simon Mwakifwamba kuungana na Tico kimtazamo.

Sambamba msanii mwingine mchekeshaji mahiri Swahilihood Steve Nyerere kuwaomba watengenezaji wa filamu wajipange ili kuirudisha tasnia ya filamu Bongo, Tico amekuwa akilalamika kutumia ujumbe wa simu wa vitisho sambamba na vitisho lakini yeye anasema bila kusema ukweli tasnia itakufa.

FilamuCentra

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364