-->

Bongo Movie Wabaguzi- Love

loveness-Watson-3

Love msanii wa filamu bongo

MWIGIZAJI wa kike katika tasnia ya filamu Loveness Watson ‘Love’ amefunguka kwa kuwalaumu wasanii wa filamu Bongo movie kuwa ni wabinafsi hawana msaada wowote katika matatizo zaidi ya wao kujiangalia na rafiki zao wa karibu ameliona hilo alivyompoteza mama yake.

“Sina hamu na Bongo Movie misiba na matatizo ni ya kwao tu lakini sisi hakuna ushirikiano wowote, mimi mwaka jana mwezi wa 12 nilifiwa na mama yangu Mbeya nikatuma ujumbe hakuna hata wa kusema pole,”anasema Love

Msanii huyo amedai kuwa amekuwa akishiriki kila msiba au ugonjwa na kuchangishwa michango yeye pamoja na kaka yake Lekonia Watson ambaye pia ni msanii lakini walipofiwa na mama yao kuna mtayarishaji mmoja tu ndio aliyekwenda Mbeya kushiriki mazishi lakini si wasanii wa Bongo movie.

FC

Comments

comments

Post Tagged with

Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364