Bushoke: Ushauri wa Mashabiki Hunijenga Sana
Bushoke amedai kuwa ushauri kutoka kwa mashabiki hasa ule anaoupata kwenye mitandao ya kijamii humjenga.
Hivi karibuni ameachia wimbo wake mpya uitwao ‘Mpita Njia’ ambao anadai kuwa mashabiki wengi wamempongeza. Akiongea na Bongo5 Bushoke amesema huwa anapenda kusoma sana koment za mashabiki wake na kuwajibu
“Unajua mimi huwa anapenda sana kusoma comment nione mashabiki wangu wanasema nini na wanatoa ushauri gani,” amesema. “Mimi huwa siogopi kusoma comment zaidi huwa napenda kuwaelewesha nikiona mtu ameuliza kitu ambacho anahitaji kueleweshwa huwa nafanya hivyo ili apate uhakika maana unajua mwingine anatamani kuonana na wewe lakini anakuwa hawezi, basi huwa nafanya hivyo kwa kuwajibu na kuwashukuru na kufanyia kazi mawazo yale ambayo naona ya muhimu,” ameongeza.
“Kuna wengine huwa wanazingua, hao huwa hawakosekani unajua ukishakuwa msanii lazima ukutane na vitu kama hivyo hasa katika mitandao. Wapo watakaokutia moyo na watakaokuvunja moyo, hizo ni changamoto tu.”
Hizi ni baadhi ya comments ambazo Bushoke alikuwa akiwajibu mashabiki wake na kuwaelewesha
Bongo5