-->

Chemical: Sijawahi Kupendwa na Stereo kwa Dhati

RAPA wa kike anayefanya vizuri kwenye Hip Hop Bongo, Claudia Lubao ‘Chemical’, amefunguka kuwa, msanii Stereo ambaye amekuwa akijanasibu kwenye vyombo vya habari kwamba anampenda, ukweli ni kwamba mwanamuziki huyo hajawahi kumpenda kwa dhati kwa kuwa bado mwanaume huyo hajamwonesha vitendo vyenye kuthibitisha hilo.

Akipiga stori na Showbiz Extra, Chemical alisema kuwa, hajawahi kupendwa kwa dhati na Stereo kwa kuwa hata siku moja, hajawahi kuelezwa kitu chochote kinachohusu mapenzi na rapa huyo, zaidi ya kumsikia tu kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

“Siwezi kujiongopea kwamba nimewahi kupendwa na Stereo, hata mara moja rapa huyo hajawahi kunipenda, nasema hivyo kwa sababu hajawahi kunifungukia live, ninaishia kumsikia tu kwenye media na mitandao ya kijamii,” alisema Chemical.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364