-->

Chid Benz Asimulia Baada ya Kumuona Diamond Akiwa Ametoboa Pua

Baada ya miezi kadhaa kutoka sober, Chid Benz jana ameachia ngoma yake mpya iitwayo Chuma aliyomshirikisha mkali wa ngoma ya Natafuta Kiki, Rayvany,kwenye kipindi cha XXL, amesimulia kwa mara ya kwanza kumuona Diamond akiwa maetoboa pua.

Chidi-Benz na diamond

Kama unakumbuka vizuri Diamond aliwahi kumuimba Chid Benz baada ya kutoboa pua kwenye ngoma aliyoimba na Nay Wa Mitego iitwayo ‘Muziki Gani’.

“Unajua sikuwa kwenye mitandao kwa muda mrefu kuna mtu alikuwa ananitumia vitu mbalimbali vinavyoendea hapa nchini, sasa alinitumia bila kuniandikia chochote, niifungua nikaangalia nikamwona Diamond lakini sikuichunguza sana, lakini baadaye akanimbia umemwona mdogo wako anaonekana anakupenda sana anakufuata kila kitu, nikamwambia mbona sijakuelewa anakiambia si umemwona katoboa pua? Ndio nikifungua nikaingalia vizuri nikaona katoboa”  Alisema Chid Benz.

Diamond843

“Sasa kuna siku nilimkuta ofisini nikamuuliza na wewe umetoboa pua? Akacheka akaniambia ametoboa” Aliongeza Chid Benz.

Cloudsfm.com

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364