Afande Sele Afungukia Sakata la Nay Kufungiwa
Msanii Afande Sele ameonyesha kutoridhishwa na kitendo cha msanii Nay wa Mitego kufungiwa kufanya kazi za sanaa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa muda usiojulikana mpaka atakapotimiza masharti aliyopewa na baraza hilo.
Afande Sele kupitia ukurasa wake wa ‘Facebook’ amesema kuwa yeye anashangaa kuona adhabu hiyo anapewa Nay wa Mitego tu ilihali kuna wasanii wengi walifanya na wanaendelea kufanya kosa kama hilo hilo ambalo amefanya Nay wa Mitego lakini wao wanaachwa na hawajachukuliwa hatua kama yeye.
“Sio jambo lakuchukiza lakini linafadhaisha pale unapojiuliza kwanini aadhibiwe yeye tu? Mbona kuna wenzake wengi tu walifanya na wanaendelea kufanya makosa kama yake au zaidi lakini hawajachukuliwa hatua kama yeye? Alihoji Afande Sele
Afande Sele alizidi kujiuliza kwanini watu wengine wanaachwa ni kwamba wana udugu, au ni wapenzi wa watu fulani fulani ndiyo maana hatua hawachukuliwi.
“Ni siasa, mapenzi, undugu au? Pole askari wangu, mdogo wangu mpiganaji, yatakwisha tu, tutawasimulia kina Shishi baby, Snurasex nk kuwa ‘hainaga ushemeji'” Alisema Afande Sele.