Da Zitta Anapenda Story Halisi Katika Filamu
MKURUGENZI wa kampuni ya Zitta Production Zitta Matembo ‘Da Zitta’ amefunguka kwa kusema kuwa siku zote anapenda kutengeneza filamu ambazo zinagusa jamii na ni hadithi halisi ambazo zinaizunguka jamii yetu kila siku na anafurahia sana kuigiza maisha halisi.
“Nilipanga kuwa ni msemaji wa wanyonge ambao hawana pa kuongelea mimi nachukua nafasi kuwakilisha mawazo yao ambayo yamewaumiza kwa muda mrefu na inakuwa faraja kwao naguswa sana na jamii na kuwatia moyo kupitia sanaa yangu,”anasema Da Zitta.
Kwa sasa anaandaa filamu kali na ya kusisimua na kuelimisha inayojulikana kwa jina la Nuru ambayo inawatia moyo watu wasikate tamaa, Da Zitta anatengeneza filamu hiyo kimataifa kwani kutakuwa na usahili kupata wasanii wenye uwezo na uhusika wa filamu ya Nuru.
Filamu yake ya Gundu inaendelea kufanya vizuri sokoni huku ikisambazwa na kampuni yake mwenyewe ya Zitta Productions ya Jijini Dar es Salaam na inapatikana nchi nzima katika maduka ya filamu Swahilihood.
Filamu Central