Davina Alia Kupoteza Jembe
Halima Yahaya ‘Davina’, staa wa sinema za Kibongo ambaye mwanzoni mwa wiki hii alimpoteza baba yake mzazi, mzee Yahaya, amesema daima atamlilia marehemu baba yake kwani alikuwa ni kiungo muhimu sana katika maisha yake yaliyobaki.
Akizungumza na gazeti hili, Davina alisema kumpoteza baba yake huyo amekuwa na maumivu makali ambayo siyo rahisi kumueleza kila mtu jinsi anavyojisikia hivyo kilichobaki kwake ni kumuomba Mungu ampe ujasiri.
“Nakuambia nimepoteza jembe maishani mwangu, najua nitaendelea kulia siku zote maana sijui machozi yangu yatakauka lini, kwa kweli roho inauma mno,” alisema Davina.
Chanzo:GPL