-->

Dawa za Kulevya Zimewashusha Wasanii- Izzo Bizness

RAPA Izzo Bizness, anayetamba na wimbo wa ‘Umeniweza’, ameweka wazi kwamba dawa za kulevya ndizo zilizoshusha viwango vya baadhi ya wasanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini.

Izzo alidai hataki kuingia ndani zaidi katika masuala hayo, lakini anaamini wasanii wengi wa muziki huo wameshuka viwango vyao vya kuimba na kutunga kutokana na matumizi ya dawa za kulevya.

“Kwa upande wangu sina mengi ya kusema kuhusu matumizi haya ya dawa za kulevya kwa wasanii, ila nawaasa hizo dawa ndizo zinazopunguza nguvu kazi za vijana na kuondoa thamani ya utu wao kwa jamii, ni bora waachane nazo kwa faida yao na nchi kwa ujumla,” alieleza Izzo.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364