-->

Jide Ataka Kulinda Heshima

MKONGWE wa Muziki wa Kizazi Kipya, Judith Wambura maarufu kama Lady Jaydee, amesema uzinduzi wa albamu yake ya saba unalenga katika kulinda heshima yake katika sanaa alikodumu kwa miaka 16 sasa.

Albamu hiyo, Woman itazinduliwa mwezi ujao katika eneo ambalo bado halijatajwa na itahusisha baadhi ya nyimbo zake zinazovuma hivi sasa kama Ndindindi, Together na nyingine ambazo bado hazijasikika.

“Ni uzinduzi wa kulinda heshima niliyoipata katika muziki, kukaa miaka 16 kileleni na kujaza watu siyo jambo dogo, nashukuru Mungu kwa hilo, jambo hili linathibitisha kuwa ninaimba nyimbo zinazoishi na tutaendelea kufanya kazi kwa nguvu ili tusiwaangushe mashabiki,” alisema Lady Jaydee.

Chanzo:GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364