Dayna: Simchukii Baba Watoto Wangu
NYOTA wa Bongo Fleva, Mwanaisha Said ‘Dayna Nyange’ amesema licha ya mambo mengi kutokea katika uhusiano wake na mwanaume aliyezaa naye mtoto wa kike, hawezi kumchukia hata mara moja.
Akichonga na Risasi Vibes, Dayna alikiri kutokuwa na mawasiliano kabisa na baba mtoto wake huyo anayedaiwa kuwa yupo Afrika Kusini, lakini ikitokea wakakutana na kumtaka mwanaye, hatasita kumpa kwa sababu ni mtu ambaye tayari wameshaunganisha damu na kutengeneza undugu.
“Unajua ni kweli kuwa katika uhusiano wangu nilipitia mambo mengi ya kuumiza yaliyosababisha mpaka tukaachana, lakini hayawezi kusababisha nikamchukia mzazi mwenzangu huyo maana tayari sisi ni ndugu,” alimaliza Dayna
Chanzo:GPL