-->

Wakali Watano wa Prof. Jay Hawa Hapa

Rapa mkongwe na Mbunge wa jimbo la Mikumi Mhe. Prof. Jay amefunguka na kutaja wasanii wake watano wa hip hop Bongo ambao anawakubali na kusema wasanii hao ndiyo wamejenga msingi na kutengeneza njia kwa wasanii wa sasa.

Prof. Jay akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio aliwataja wasanii hao kuwa ni pamoja na kundi la ‘Kwanza Units’, Hard Blasters, Sugu, Fid Q pamoja na rapa Hashim Dogo ambaye amekuwa akitajwa na wasanii wengi wa hip hop wakionesha kutambua uwezo wake na mchango wake katika muziki wa hip hop Bongo.

Prof Jay siyo wa kwanza kumtaja Hashim Dogo kama msanii anayekubalika, wasanii wengine wa hip hop ambao tayari walikwisha kiri kumkubali rapa huyo ambaye amepotea kwenye ulimwengu wa bongo kwa sasa, ni pamoja na Fid Q, One The incledible, Nikki Mbishi na wengine wengi.

Mbali na hilo Prof. Jay alisema kuwa huwezi kutaja hip hop ya Bongo ukashindwa kumtaja rapa Mr. Two alimaarufu kama Sugu ambaye sasa ni Mbunge wa jimbo la Mbeya Mjini na kusema kuwa Sugu alifungua milango kwa kufanya show kubwa nje ya nchi miaka hiyo na kufanya muziki wetu uweze kupenya zaidi sehemu zingine.

“Hawa niliowataja hapa ni kati ya watu ambao wamefanya kazi ya kuchonga barabara kwa muziki wetu wa hip hop hivyo saizi hawa wasanii wa sasa wanapita ila kazi kubwa ilifanywa na watu hawa” alisema Prof. Jay

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364