Dhamira Ndiyo Siri ya Kuacha Madawa-Dudubaya
Msanii wa Bongo Flava Dudubaya amesema ili mtu aweze kuacha madawa ya kulevya ni hadi dhamira yake imsute na kuamua mwenyewe kwa dhati.
Akizungumza katika kipindi cha FNL kinachorushwa na EATV, Dudubaya amesema msanii mwenzake Chid Benz na wasanii wengine hawawezi kuacha kutumia madawa ya kulevya kwa watu kuwapeleka popote kama dhamira yao haijawasuta kuhusu jambo hilo.
“Kama una mtoto ambaye ni changudoa hata ufanye nini kama dhamira yake haijamsuta akaamua kwa dhati kutoka moyoni mwake hataacha atakuwa anaruka hadi ukuta ndivyo ilivyo kwa watu ambao wameshajiingiza kwenye madawa ya kulevya” Amesema Dudu Baya.
eatv.tv