Tetesi za Harmonize na Raymond Kuvimbiana,Memeja Afunguka
Meneja anayewasimamia wasanii wa WCB wakiwemo Harmonize na Raymond, Ricardo Momo, amekanusha tetesi kuwa mafahari hao wamekuwa wakivimbiana na kwamba kila mmoja anajiona bora.
Akiongea na mtangazaji wa kipindi cha Supa Mega cha Kings FM ya Njombe, Prince Ramalove, Ricardo amedai kuwa wawili hao wanaishi kwa upendo mkubwa.
“Hayo ni maneno tu, sisi tunaishi kama ni familia moja, natamani siku moja uje uone tunavyoishi, tunataniana , tupo kwenye shida tunasaidizana,” amesema.
“Hakuna hata mmoja mwenye ugomvi na mwenzake, hayo ni maneno tu ya watu wa nje, hakuna matatizo yoyote yaliyotokea kati ya Harmonize na Raymond.”
Sikiliza hapa