Diamond Afunguka Kuhusu ‘Salome’ Ilivyowavuruga Wizkid, Teckno na NeYo
Msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz ambaye kwa sasa anavizuri na wimbo wake ‘Salome’ amefunguka na kusema kuwa wimbo huo uliwavuruga wasanii wengi wakubwa duniani kabla hajatoka hata baada ya kutoka.
Diamond Ploatnumz alisema hayo kwenye Friday Night Live (FNL) na kudai kuwa wimbo huo yeye mwenyewe anashindwa kuelewa una nini kutokana na jinsi ambavyo umeweza kupokelewa vizuri na kupendwa na watu wengi sana duniani.
“Kiukweli kabisa hata wakati napata wazo kusema nifanye wimbo wa ‘Salome’ nilikuwa nasema ni wimbo fulani mzuri kiasi kwamba hata mtu asipoelewa lugha lakini anaweza kuipenda, nikumbuka hata wakati Mama yule Said Karoli alipoimba wimbo ule na ulipokuwa unavuma tulikuwa hatuelewi anazungumza nini lakini tuliipenda na ilikuwa nzuri na ilivuma sana, kwa hiyo nikasema kwa sasa hivi soko lilivyokuwa na nikiwatizama Watanzania nikichukua wimbo ule nikatia vitu vyangu fulani hivi itakuwa kali zaidi. Saizi wimbo huu Afrika na sehemu ambazo wanatutizama imekuwa kubwa nafikiri watakuwa wameipenda sana hata ukiangalia ‘Comments’ zao kwenye video ile ‘Youtube’ unaona kuwa wameipenda. Kabla ya wimbo kutoka Wizkid alikuwa Tanzania wakati nipo naye nilimpa ule wimbo aisee ulimvuruga sana, nilipata bahati ya kuwa na Mheshimu Rais Mstaafu Jakaya Kikwete naye aliupenda sana, hata baada ya wimbo kutoka wasanii wakubwa kama wakina Teckno, Flavour walinitumia ujumbe mfupi kuonyesha kupenda nakumbuka hata Neyo naye aliniambia ‘I like the song'” alisema Diamond Platnumz
eatv.tv