Mashabiki Wanadhani Nimeacha Kuigiza – Shamsa Ford
Malkia wa filamu Shamsa Ford amesema anapokea maswali mengi kutoka kwa mashabiki wake wakimuuliza kama ni kweli ameacha kuigiza baada ya kuingia kwenye maisha ya ndoa.
Mwigizaji huyo ambaye alifunga ndoa mwezi mmoja na nusu uliopita na mfanyabishara wa maduka ya nguo, Chidi Mapenzi, amesema ndoa haiwezi kumtenganisha na mashabiki wake wa filamu.
“Kusema kweli toka nifunge ndoa mashabiki wangu wamekuwa wakiniuliza kama nitafanya tena filamu, wengine wanasema nimeacha kuigiza,” alisema Shamsa. “Jamani mimi bado nipo sana kwenye filamu, nisingekuwa Shamsa bila filamu, kwa hiyo kuna mambo mazuri mengi yanakuja,”
Mwigizaji huyo amesema ‘Chale Mvuvi’ na ‘Dhamana’ ni filamu zake mpya ambazo zitaingia sokoni hivi karibuni na kukata kiu ya mashabiki wake wa filamu.
Bongo5