Diamond Awapa Makavu Watu Hawa
Diamond Platnumz amewatolea povu watu wanaokosoa kitendo cha yeye kula ‘Good time’ na mama watoto wake Zari the boss lady kwa madai kuwa mwanamama huyo ametoka kwenye majonzi ya kufiwa na mama yake siku sio nyingi.
Kupitia mtandao wa instagram, Diamond aliweka picha hiyo hapo juu nakufunguka;
“Kuna vichupi kunuka wanajifanya wanajua sana uchungu wa Misiba ya watu…. Mtoto wa watu katoka katika matatizo mfululizo, anatakiwa apelekwe sehem tulivu apetiwepetiwe adekezwe apate faraja!…sasa kama nyie hamna mabwana wa kuwafanyia hayo, Msijifanye ni Tamaduni na kulazimisha kila mtu awe kama nyie, eti kutwa nzima ajifungie chumbani kulia… Pambaneni na Mahusiano yenu…! Nina siku 5 za kumpetipeti… leo ndio kwanza Ya kwanza ?.” ameandika Diamond Instagram.
Diamond amefikia hatua hiyo baada ya watu kumponda mpenzi wake Zari The Boss Lady, ambaye siku ya jana alikuwa Instalive na mkali huyo wa Eneka wakijiachi kimahaba, hali iliyofanya mitandao ya kijamii kumponda kuwa anaonyesha hana uchungu wa kufiwa na mzazi wake, kazi yake ni kujiendekeza na mapenzi.