Diamond, Belle9 Wambeba Saida Kalori
WASANII wa Muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Abednego Damian ‘Belle9’ wamembeba msanii mwenzao anayeimba nyimbo za asili, Saida Kalori kwa kushiriki katika albamu yake itakayoitwa Naamka.
Akilonga na Showbiz, Saida aliyewahi kutamba na Wimbo wa Chambua Kama Karanga ‘Maria Salome’ alisema kuwa anamshukuru Mungu amerudi tena kwenye gemu na wasanii hao wamempa nguvu ya kufanya vizuri katika albamu
hiyo.
“Nimeamka tena jamani nashukuru nimebebwa na wasanii wenzangu Diamond na Belle9 ambao nimewashirikisha kwenye nyimbo zangu ambazo zipo kwenye albamu itakayotoka hivi karibuni,” alisema Saida.
Kwa nyakati tofauti Belle9 ameachia Wimbo wa Give It To Me ambapo ndani yake ameweka vionjo vya Wimbo wa Chambua Kama Karanga wakati Diamond naye amefanyia ‘remix’ ya wimbo huo wa Saida kwa kuita jina la Salome
Chanzo:GPL