-->

Harmorapa Afungukia Kilichomtoa Mbio kwa Nape (VIDEO)

Msanii asiyekaukiwa ‘kiki’ katika ulingo wa sanaa ya Bongo, Harmorapa amesimulia kilichomkuta alipokwenda kumuona aliyekuwa Waziri wa habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye kiasi cha kutoka mbio za aina yake, baada ya kuona bastola.

Harmorapa ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake inayokwenda kwa jina la ‘Kiboko ya Mabishoo’ aliyomshirikisha Juma Nature, amesema kilichomfanya aende katika mkutano ule mara baada ya Nape kuondolewa kwenye nafasi yake ya uwaziri, ni kumpa pole na kumshukuru Nape kwa kuwa ndiye aliyekuwa mlezi wa tasnia ya sanaa nchini.

Akizungumzia tukio alilolishuhudia la Nape kutishiwa bastola mbele yake, Harmorapa aliyekuwa akizungumza na eNewz ya EATV, amekiri kuwa ni kweli hajawahi kuiona kwa ukaribu ule, hivyo alipoona inachomolewa aliogopa na kujikuta akitoka mbio, huku akikanusha utani ulioenea mitandani kuwa alikimbia hadi Mtwara.

Mtazame hapa chini akifunguka kupitia kipindi cha eNewz

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364