-->

Diamond Kama Vipi Malizia Bongo Muvi

NIMEKUWA nikikagua kwa umakini sana video za wasanii mbalimbali hususan wa Bongo Fleva katika ubora wake ili kujiridhisha kama bajeti za kushutia wanazozitaja zinalingana na ukweli halisi kwa kuzingatia mambo mbalimbali ya kiweledi.

diamond3422

Kwenye kwaliti sio inshu lakini kwenye uhalisia ndiyo inshu na kichupa kikibamba na kuwa poa kwa levo inakuwa njema, kinapagawisha na kila mida unataka kukikagua manake hakikuchoshi.

Nimegundua kitu katika video za Diamond Platnumz tangu alipoanza kitambo chake (back) hadi kufikia levo yake ya sasa (front), mabadiliko ni makubwa katika kutendea haki vichupa vyake kwa jinsi anavyoshuti manake tangu mida ile ya ‘Kamwambie’ kisha kupitia ‘Mbagala’ na baadaye ‘My Number One’ hadi kudondokea kwenye ‘Utanipenda?’.

Si tu katika ubora unaoridhisha lakini kikubwa ni simulizi kueleweka hata kama utapima kwa vigezo vya kiweledi zaidi, kimojawapo ni kukicheki kichupa kimya kimya na kama ‘scenes’ zinaleta stori inayoeleweka basi hiyo ni mukide kabisa.

Lakini engo nyingine ni hisia na kuigiza matukio ambapo Platnumz wa zamani na wa sasa kadiri anavyoendelea ni tofauti, kama ulivyomuona katika ‘Utanipenda’ alivyoigiza ukachala hata zile ‘gesture’ yaani hisia za usoni zinajiakisi inavyopaswa.

Kwa levo hiyo ya uwezo wa kukubalisha simulizi kwenye kichupa kwa kujikita vyema kuigiza matukio yanayohusika safari yako Diamond uliyoianzia ‘Mbagala’ haipaswi kuishia kwenye vichupa tu, kwa nini usiende matawi mengine ukaigiza muvi kabisa wewe kama wewe kwa stori ya kivyako na songi zako zikawa soundtraki za kusindikizia matukio ya hiyo muvi!?

Kule mbele kwa wenzetu waliotutangulia ni kawaida kabisa msanii wa mikong’osio kujikita kwenye muvi manake muvi nazo bila nyimbo haziendi kwani zitaboa, basi kama ni hivyo hata hapa kwetu inawezekana sio kwa kushirikishwa vipande flani tu lakini kuwa muvi kamili ya kwako mwenyewe msanii husika.

Manake iko hivi kwako Almasi a.k.a Diamond kwa Kitasha, kama ni mshale ulioibuka zama zile (back) ukakitwa lakini hadi sasa bado unapaa kwenye levo nyingine (front) basi mshale upae zaidi, kwa kuchupa kwenye kiwango kingine itadhihirisha kuwa ulipofikia sio mwisho wa vidato unavyopaswa kukwea.

Inapendeza kukwea levo kwenye nyanja mbadala manake umethibitisha mauwezo yako kwa kuwapiga tafu wengine kupitia WCB hadi wale wa levo yako wasiomaindi watu kuchonga wametinga kwenye lebo yako akiwemo Rich Mavoko.

Sasa kama ni hivyo basi songa huku kwenye levo mbadala ushushe muvi moja au mbili inatosha manake vichupa vyako vinajieleza, kwamba ukiongozwa na muongozaji mwenye uwezo kama ilivyo kwenye vichupa basi haina shaka kuwa itakuwa poa na kitu kitakachoibuka kitakuwa mwake mwake kabisa babake mwenyewe.

Inawezekana ni kujipanga tu kukamilisha inshu hiyo ambayo inakuchagiza uitimize kisha kila kitu kitakuwa levo nyingine mpya manake hiyo ndiyo ‘front’ unayopaswa kuifikia kutokea ‘back’ uliyotoka kitambo kile.

Kwa sasa tatizo sio Mbagala na umehama Tandale ukiishi Madale na bila shaka watu wako watakupenda zaidi ukitia maguu kwenye Bongo Muvi.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364