-->

AISHA BUI Kimya Changu Kina Mshindo

BAADA ya kimya cha takribani miaka mitatu, msanii wa filamu za Kibongo, Aisha Bui ameibuka na kudai kuwa, mashabiki wake wajiandae kumpokea kwa kazi nzuri, zenye kusisimua.

aisha-bui

Akipiga stori na Gumzo la Town, Aisha Bui ambaye aliibuliwa na Filamu ya My Book iliyotayarishwa na mwigizaji nguli Deogratius Shija, ameeleza sababu za kukaa pembeni kwa muda ni kumlea mwanaye.

Kabla ya kuingia kwenye filamu, Aisha alipata umaarufu baada ya kuolewa na mfanyabiashara maarufu Bongo, marehemu Mohamed Mpakanjia ‘Meddy’ ambaye pia alipata kuwa mume wa marehemu Amina Chifupa, aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM) na mtangazaji wa redio.

“Kwa sasa nimeolewa na nina mtoto mmoja wa kike aitwae Paloma, nashukuru Mungu mume wangu ananisapoti kwa kazi yangu ingawa mwanzo ilikuwa changamoto sana. Hakutaka niendelee na sanaa.

“Alinikataza kwa sababu mume wangu alikuwa hataki kabisa kusikia  skendo, maana baadhi ya wasanii wanaandikwa sana magazetini kwa skendo. Hiyo ilimtisha sana. Lakini nilimshawishi na alikubali.

“Hata hivyo akiwa amenikubalia, Mungu akaleta neema nyingine ya ujauzito, ikabidi nijipe likizo ya uzazi. Tayari mwanangu sasa ameshakua kidogo, ndiyo maana nimeamua kurudi kwenye game kwa nguvu mpya,” anasema Aisha ambaye sinema ya Saturday Morning aliyocheza na marehemu Steven Kanumba ilimuweka pazuri kwenye tasnia ya filamu za Kibongo.

UJIO MPYA

Aisha anasema, baada ya kushiriki filamu nyingi za watu, ameshasajili kampuni yake na sasa naye ni mtayarishaji huku akijipanga kuanza kusambaza kazi zake mwenyewe.

“Kampuni yangu ni Bad Girl, tayari nimeshatoa filamu ya Mshale wa Kifo ambayo nimemshirikisha Gabo Zigamba, kwa sasa niko jikoni nakuja na vitu vingine vizuri zaidi na ninaamini nitawakonga nyoyo mashabiki wangu,” anasema na kuongeza:

“Lengo langu kuu ni kuanza kusambaza filamu zangu mwenyewe. Nawashauri wasanii wenzangu tusibweteke, tusambaze wenyewe kazi zetu maana naamini tunaweza, tuachanane na hali ya kudhulumiwa, hakika tukishirikiana tunaweza.”

“Naamini wasambazaji ndiyo wanaotupoteza na kutufanya tuishi maisha ambayo siyo yetu,”

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364