-->

Diamond Kutoa Album ya Kimataifa

Msanii Diamond Plutnumz amekusudia kuondoa kiu ya watu wengi kwenye game la bongo fleva, kwa kutoa album ya nyimbo zake.

DIAMOND7812

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Diamond amesema amekusudia kuwa kabla ya mwisho wa mwaka huu atatoa album ambayo itabeba nyimbo zenye ubora wa kimataifa, na kuondoa ukimya wa kutotoa album.

“Mwaka huu kabla ya kuisha naenda kutoa international album kwa sababu natazamwa na nchi tofauti tofauti, itakuwa album ya kwanza kuitoa kiinternational, zamani management yangu ilikuwa inakataa kutoa album, ikisema utatoa album alafu unauza ndani tu ndio nini sasa, tunataka ukitoa album iuzwe kama inavyouzwa album za kina Usher huko, sasa hivi na mimi nipo kimataifa, so nitatoa album”, alisema Diamond.

Pamoja na hayo, Diamond amewataka watu waelewe kuwa muziki anaoufanya anafanya kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi, ili kuwatimizia watanzania kile wanachokihitaji na aina ya muziki wanaoupenda, huku pia akilenga kupata soko la kimataifa, na ndiyo maana kuna nyimbo zingine hapa ndani hazihit lakini kimataifa zinafanya poa, na nyingine zinafanya vizuri zaidi hapa nyumbani.

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364