-->

Alikiba na Mr Blue Kumrudisha Abby Skillz

Msanii Alikiba na Mr Blue ambao wote wanafanya vizuri kwa sasa kwenye muziki wa bongo fleva wameshirikishwa kwa pamoja kwenye wimbo mpya wa msanii Abby Skillz ambao unategemewa kutoka siku za karibuni.

Alikiba

Msanii Alikiba akiwa na Abby Skillz wakati wakitengeneza video ya wimbo mpya wa Abby Skillz.

Kutokana na kipande kidogo ambacho ameimba Alikiba kwenye wimbo huo, kimepokelewa vizuri na mashabiki ikiwa ni ishara kwamba wimbo huo utafanya vizuri na kumrudisha kwenye ramani ya muziki msanii Abby Skilliz ambaye kwa muda mrefu alipotea kwenye soko la muziki.

Baadhi ya mashabiki walitoa sifa nyingi kwa Alikiba baada ya kusikia kipande hicho huku wengine wakimtania kwa maneno ya furaha kuwa anaimba kwa sifa wakiwa na maana anaimba vyema kiasi cha kukonga nyonyo zao.

“Narudia tena acha sifa kaka, sasa unataka wengine tuimbe nini kaka? sa hizi mimi naacha harakati za kuimba maana pakutokea hapapo. Kiba umebana hadi penati” alisema Afredy Ilomo

Alikiba 2

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364