Diamond na Mr Blue Wananibeba – Dully Sykes
Msanii mkongwe wa muziki wa bongo fleva Dully Skyes amefunguka na kusema kuwa katika wasanii wote ambao aliwasaidia katika muzuki mpaka wametoboa ni wasanii watatu tu ambao wamekuwa wakilipa fadhila kwake na ambao wamekuwa wakimpigania.
Dully Skyes alisema hayo kwenye kipindi cha Planet bongo na kusema kuwa amewasaidia wasanii wengi lakini wengi wao wamekuwa wakiishia kumuita Braza D tu ila Diamond Platnumz, Mr Blue pamoja na Queen Darlin ndiyo wasanii pekee ambao wamekuwa wakilipa fadhila kwake pamoja na kumpigania.
“Watu ambao nimewasaidia wananipa heshima ni wawili tu, wengine wanaishia kuniita braza D tu, lakini Diamond Platnumz, Mr Blue pamoja na Queen Darlin ndiyo wananipa ile heshima kabisa na wanauchungu na mimi kwamba huyu kaka yetu kwa hiyo katika wale watoto ambao nimewatoa kwenye muziki wakiwa wadogo na wananisaidia ni hao watatu” alisema Dully Skyes