-->

Diamond Platunumz afunguka mazito kuhusu mtoto wa Hamisa Mabeto

Dar es Salaam. Mwanamuziki Diamond Platnumz amesema uhusiano wake na mwanamitindo Hamisa Mobeto umeidhalilisha familia yake hasa mama yake na mzazi mwenzake Zarina Hassan, maarufu Zari.

Akizungumza katika kipindi cha Leo Tena kinachorushwa na kituo cha Redio cha Clouds jijini Dar es Salaam leo Jumanne, Diamond amesema mama yake alitukanwa katika mitandao ya kijamii baada ya kumtembelea mwanamitindo huyo alipojifungua takribani wiki sita zilizopita.

“Nilimwomba mama yangu aende akamwangalie mtoto ingawa hakuwa amefurahishwa na tukio zima, nilimwambia mama yule ni mtoto wangu hana jinsi inabidi tu akamwangalie lakini alipokwenda mwenzangu aliwaita watu wampige picha na baadaye alidhalilishwa,” amesema Diamond.

Diamond amesema mbali na mama yake tukio hilo limemdhalilisha mzazi mwenzake kwa kuwa picha na video zilizokuwa zikitolewa zililenga kumuumiza.

“Zari hana hatia katika hili, haya yote yanatokea kwa sababu ya ujinga wangu, maskini yangu wote wameingizwa katika mkumbo na kudhalilishwa, namshukuru Mungu nilimweleza ukweli wote mzazi mwenzangu naye akanielewa,” amesema Diamond.

 

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364