-->

AliKiba Awashangaa Wanaompakazia Amekopi Seduce Me

Wakati Seduce me ikiendelea kukimbiza ambapo mpaka sasa imeweza kufikisha watazamaji milioni tano na kuahidi kuachia dude jipya endapo itafikisha watazamaji milioni kumi, Ali Kiba amewatolea povu watu wanaodai kuwa wimbo huo amekopi kutoka kwa jamaa huko ufilipino.

“Kitu kizuri siku zote huwa kinapigwa mawe, wimbo huu ni wa kisasa ndio maana watu wanaongea sana na mimi nawaacha waongee ila wimbo sijakopi sehemu yoyote tu.”

“Kukopi wimbo kwangu haiwezekani na haitakuja kutokea kamwe, sababu huu wimbo nilianza kuandika huu wimbo kutoka Studio ila najua kuna watu wanataka kuuzima wimbo, sasa kwanini wanataka kuuzima wimbo wakati wa watu huu,” aliongeza.

Pia Kiba aliongeza juu ya uwezekano wa kutokea kwa Remix ya Seduce Me lakini hayo amesema bado yapo chini ya mipango na kama itatokea basi mashabiki zake wataona kila kitu.

“Pia kuna mipango ya kolabo na G Nako na kama itatokea Remix ya Seduce Me nitapenda pia tena natamani wasanii wote waweke sauti zao,” aliongeza.

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364