Diamond, Zari Walipamba Jarida Maarufu la Sauzi
MWANAMUZIKI mwenye taito kubwa kwa sasa nchini na Afrika, mtoto wa Tandale na Mkurugenzi wa Kampuni ya Wasafi Classic Baby (WCB), Nassib Abdul ‘Diamond Platnumz’ na mzazi mwenzake, Zarina Hassani ‘Zari’ wamelamba shavu kubwa baada ya kuvuta mkataba wa kupiga picha za kupendezesha jarida maarufu la Afrika Kusini liitwalo ‘Papas and Mamas’.
Kitendo hicho kimewafanyanyote hao kuingia katika rekodi moja na hayati Nelson Mandela Madiba ambaye naye aliwahi kuandikwa sana katika jarida hilo.