-->

Hawa Ndiyo ‘Marapa’ Watano Anaowakubali Roma Mkatoliki

Rapa Roma Mkatoliki leo kwenye kipindi cha Planet Bongo amefunguka na kutaja orodha ya wasanii wake wa tano wa hip hop Bongo ambao anawasikiliza na kuwakubali zaidi kutokana na kazi zao.

Roma Mkatoliki kwa kuanza alimtaja Rapa Roho Saba na kusema anamsikiliza sana na kumkubali sana na watu watashangaa kwanini amemtaja Roho Saba ili hali ana ngoma mbili tu ila yeye anasema anazisikiliza sana hizo kazi mbili kuliko kazi nyingine nyingi kutoka kwa wasanii wengine.

“Kiukweli nawasikiliza sana wasanii wengi wa Hip hop Bongo lakini kwa kuwa nimepewa nafasi ya kutaja wasanii watano tu wa kwanza nitaanza na mwanangu Jaco Roho Saba, mchizi ana ngoma mbili tu lakini nazisikiliza sana, namkubali sana Jose Mtambo, Prof Jay pia maana kitambo namsikiliza na alini’inspire’ toka enzi hizo mpaka leo. Wengine ni Saigoni pamoja na Hashim Dogo” alisema Roma Mkatoliki

eatv.tv

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364