Dino Arudi Kuikoa ‘Bongo Movie’
Msanii wa Bongo Movie Dino amesema kwa sasa yupo tayari kurudi kwenye tasnia hiyo baada ya kukaa miaka minne bila kucheza movie yeyote hali iliyofanya ajifunze mengi nje ya movie.
Akipiga story kupitia eNewz, Dino amesema hawezi kupotea kwenye movie kwa kuwa alikuwa anafanya vizuri na ana kipaji ambacho yeye mwenyewe anakitambua hali inayopelekea mashabiki zake kuendelea kumkumbuka kwa kipindi chote ambacho hajatokea kwenye movie.
Dino amesema kwa sasa anaangalia mashabiki wanataka nini kwa kutoa movie nzuri na kurudisha hadhi ya bongo movie kwa kuwa yupo kwenye movie tangu mwaka 1999.
eatv.tv