Dogo Janja Afungukia Kuoa
SIKU chache baada ya Mbongo Fleva, Khalid Ramadhan ‘Tunda Man’ kufunga ndoa, mwanamuziki mwenzake, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ (pichani juu) ameibuka na kumpongeza huku akieleza kuwa naye yupo mbioni kufuata nyayo zake.
Dogo Janja amefunguka kuwa Tunda Man ameushinda ujana, kitendo kinachomfanya yeye kutamani kufikia hatua hiyo, endapo mambo yataenda vyema, Februari mwakani itakuwa zamu yake.
“Tunda amenishawishi sana kuoa, Februari mwakani nitaoa, maana umri unaruhusu, nitaoa mwanamke wa kawaida, siyo msanii,” alisema Dogo Janja.
Chanzo:GPL