Dogo Janja na Irene Uwoya Wasisikilize Maneno ya Watu-Madee
Msanii Madee Seneda ambaye ni baba mlezi wa Dogo Janja, amewataka maharusi wake Irene Uwoya na Dogo Janja kutosikiliza watu kwani wakifanya hivyo hata mwaka hawatamaliza.
Madee ameyasema hayo alipokuwa akipiga stori na Queen Fifi na JR kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwamba amefurahi kuona Dogo Janja kaoa ingawa alishtushwa na taarifa hizo, lakini kikubwa ni kuwaombea ili wasisikilize maneno ya watu.
Madee ameendelea kusema kwamba wawili hawa wote ni watu maarufu hivyo kutakuwa na maneno mengi kutoka kwa watu, na iwapo wakisikiliza basi ndoa yao haitafika mbali.
EATV.TV