-->

Maombi Yatikisa Nyumbani kwa Lulu

Zikiwa zimesalia siku 12 tu kabla ya hukumu yake kusomwa kufuatia kesi yake ya kuua bila kukusudia inayomkabili, taarifa zinasema maombi na sala zimekua zikitikisa nyumbani kwa msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Mtu wa karibu wa msanii huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake, alilidokeza Risasi Mchanganyiko kuwa, baada ya kesi hiyo kufikia katika hatua ya hukumu, hivi sasa kila siku maombi yanafanyika asubuhi, mchana na jioni, kwani kwa hali ilivyo hivi sasa, kila kitu kimo mikononi mwa Mungu.

“Si Lulu, si Mama yake, si ndugu zake, kila mmoja anaomba kwa muda wake, wakati mwingine kwa pamoja, au mmoja mmoja, wanachojua wao hatima ya kila kitu ipo mikononi mwa Mungu, ndiyo maana sala zinaelekezwa kwake,” alisema mtu huyo.

Lulu anashtakiwa kwa kosa la kumuua bila kukusudia, aliyekuwa mpenzi wake, Steven Kanumba, katika tukio lililotokea nyumbani kwa msanii huyo, Sinza Vatican mwaka 2012.

Baada ya kusikilizwa kwa ushahidi wa Jamhuri, upande wa utetezi na wazee wa mahakama, sasa hukumu hiyo itasomwa Novemba 13, mwaka huu katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Jaji Sam Rumanyika.

Chanzo;GPL

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364