Dr Cheni Aachana na Bongo Movie Kwasasa, Hii Ndiyo Sababu
Staa mkongwe wa Bongo Movie, Dr Cheni amefunga kuwa kwasasa hata cheza tena filamu hadi pale serikali itakapo hakikisha kuwa filamu zao zinalindwa dhidi ya wizi wa kazi zao.
Akiongea na Enews ya EATV, Dr Cheni alisema kuwa usalama wa kazi zao ndiyo tatizo kwenye tasnia ya bongo movie
“ Siwezi kutoa tena filamu hadi Serikali itakapo hakikisha kuwa kazi zetu zipo salama, ukitoa filamu leo siku moja ya pili ya tatu unazikuta chini zinauzwa feki . Kiio chetu sisi bingo movie ni kazi zetu zinaibiwa namuomba Rais Magufuli aingilie kati swala hili kwani vijana wengi wamejiajili kwenye bongo movie.” Alisema Dr Cheni