-->

DSTV Kuwapa Ulaji Waigizaji wa Bongo Movies

KING’AMUZI cha Dstv kilicho chini ya Multchoice, kinatarajia kutoa kipaumbele kwa waigizaji Watanzania kutumia chaneli yake ya ‘Maisha Magic Bongo’ kutoa elimu ya lugha ya Kiswahili Afrika.

Barbara Kambogi

Barbara Kambogi

Akizungumza na MTANZANIA jana, Barbara Kambogi alisema watakuwa wakitumia kazi za waigizaji wa Tanzania kufundisha lugha hiyo.

Barbara alisema kuwa Ijumaa ijayo wanatarajia kufanya mazungumzo na waigizaji wa Tanzania, ili kuwapa utaratibu mzima wa kuwakilisha kazi zao katika kituo chao kilichopo nchini Kenya.

“Maisha Magic Bongo ni chaneli ambayo imepata umaarufu Afrika na nje ya Afrika, watu wengi wasiojua Kiswahili wamekuwa wakijifunza kupitia filamu zinazoonyeshwa,” alisema Barbara.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364