-->

Duma Afunguka Haya Kuhusu Picha zake Tata

INAKUWAJE Pale ambapo unakuwa na hamu ya kutoka kimapenzi na mtu maarufu harafu hupati nafasi hiyo kufuatia staa unayemtamani yupo kwenye penzi zito na mtu mwingine? Bila shaka picha zake zinaweza kuwa tulizo lako tosha.

Ukubwa wa majina ya mastaa unaongeza idadi ya mashabiki wanaotamani kutoka nao kimapenzi ila hawapati fursa hiyo kwa sababu tu ya umbali na ugumu wa kukutana na mastaa hao.

Mara nyingi wasanii wakike hupiga picha za utupu na kusisambaza kwenye mitandao ya kijamii kwa lengo la kusaka kiki na kukata kiu ya mashabiki wa kiume wenye mawazo ya kuja kutoka nao kimapenzi.

Ni nadra mtu maarufu wa kiume kupiga picha zinazoonyesha sehemu kubwa ya mwili wake kwa lengo la kuwaridhisha watoto wa kike ambao wamekuwa wakimsumbua kwa kumtaka kimapenzi.

Wiki hii Chombezo Tata limekutana na staa wa filamu za kibongo Daudi Michael ‘Duma’ ambaye wiki jana kwenye mitandao ya kijamii zilisambaa picha zinazoonyesha sehemu kubwa ya mwili wake.

Picha hizo zimepokelewa kwa mitazamo tofauti na mashabiki ambao walianza kumuona toka akiwa kwenye tamthilia ya Siri ya Mtungi na ile ya Nira aliiyofanya nchini Kenya hali kadharika katika filamu kama Mchongo Siyo, Mfadhili Wangu  na Chutama.

AZITOLEA UFAFANUZI

Baada ya Chombezo Tata kumuweka kikaangoni, Duma anasema yeye ni mwanamitindo ambaye ameshafanya matangazo kadhaa na kampuni mbalimbali na zile picha zilizovuja mtandao zilikuwa ni kwa ajili ya moja ya kazi zake.

Na jambo la kushangaza zaidi picha hizo ziliwafurahisha wanawake wengi waliokuwa wanamsumbua kwa kumtaka kimapenzi, wengi wao walimpigia simu na kumpongeza kwa kuwa ziliwavutia.

“Najua watu wameni tafsiri vibaya ila nashukuru baada ya picha zile kusambaa, simu za wanawake waliokuwa wananitongoza zimepungua, kwani wametumia picha zangu kwa kujiliwaza na kumaliza matamanio yao hivyo sitegemei tena kusumbuliwa kama zamani,” anasema Duma.

LENGO LAKE HASA

Duma anasema hii ni dunia ya utandawazi, watu maarufu wanapendwa kimapenzi na watu wengi hivyo njia rahisi ya kukata kiu ya maelfu ya mashabiki warembo/watanashati ni kuwapa fursa ya kuwa picha hizo za utupu.

“Nchi nyingi zilizoendelea mastaa wanafanya hivi, ili kulinda afya zao na kuepusha skendo za kutoka na wanawake au wanamume wengi, hii ni njia rahisi ya kumsaidia yule mwanamke ambaye hawezi kunifikia, nimeonekana mtu wa ajabu ila nalinda afya na jina langu,” anasema Duma.

MPENZI NA FAMILIA YAKE JE?

Mkali huyu anasema kwa sasa yupo singo japo kuwa ni baba wa watoto wawili ila upande wa familia yake jambo hilo walilipokea vibaya lakini aliwaelewesha wakaelewa.

“Hakuna ndugu anayependa ndugu yake aharibikiwe au afe kwa maradhi kwa hiyo mimi nina sababu za msingi za kufanya hivyo ndiyo maana familia yangu ikanielewa pia,” anasema.

AJIBU VIJEMBE VYA MASHABIKI

Duma anasema amepokea maoni mbalimbali ya mashabiki ila kwa wale waliomuelewa vibaya na kumtukana wanapaswa kufahamu kuwa yeye anajitambua na endapo asingefanya hivyo na kushiriki ngono na wanawake wengi pia wangemtukana.

“Najua watu wamelipokea tofauti jambo hili ila ningekuwa na mademu wengi pia ingekuwa ni tatizo na pia siwezi kufanya jambo likampendeza kila mtu aliyeelewa ameelewa na atakayechukia basi acha achukie,” anasema.

KAZI KAMA KAWA

Anasema yeye ni msanii wa kwanza wa filamu anaye washirikisha mashabiki kazi zake kabla hazijatoka na kuvutia kampuni mbalimbali kutangaza kwenye filamu zake anazoziweka katika chaneli yake ya Youtube.

Mtanzania

Comments

comments


Unataka kutangaza nasi? Tumia namba ya simu hapo chini.

Please contact us: email : info@bongomovies.com or Mobile: +255 756 348 364