Erycah: Wema, Uwoya Kaeni Chonjo
VIDEO Queen ‘hot’ Bongo ambaye ameonekana kwenye video za wasanii mbalimbali wa muziki, Ericka Daniel ‘Erycah’ amefunguka kuwa, mastaa kama vile Wema Sepetu, Irene Uwoya, Elizabeth Michael ‘Lulu’ na wengineo wakae chonjo kwani amedhamiria kufunika ustaa wao.
Akipiga stori na Ijumaa juzikati, Erycah ambaye hivi karibuni aliing’arisha Video ya Kwa Hela ya Mwanamuziki Linex alisema, yeye anajijua ni mzuri ndiyo maana ameanza kusumbua kwenye mambo ya umodo na anatarajia kuingia kwenye uigizaji ambako anaamini atafanya poa pia.
“Nilishawahi kufanya filamu huko nyuma lakini nikatulia kwanza, sasa nimeingia kwenye muziki kwa kuwa video queen, hawa akina Lulu Diva, Gigy Money na Kidoa wala siyo levo zangu, wanaoweza kushindana na mimi kwa umbo na sura ni akina Wema, Uwoya nao pia wakae chonjo kwani muda wangu wa kung’ara ni huu,” alisema Erycah.
Chanzo:GPL